Mabadiliko kwa kifupi ya vizuizi

Ikiwa una wasiwasi, piga simu laini ya simu ya coronavirus 1800 675 398 (masaa 24).
Ikiwa unahitaji mkalimani, pigia simu TIS National kwa nambari 131 450.
Tafadhali tumia Sufuri Tatu (000) kwa dharura pekee.

Kile unapashwa kukumbuka

 • Unapashwa kuvaa kifuniko cha uso wakati unapotoka nyumbani.
 • Jiweke umbali wa usalama wa angalau mita 1.5 kutoka kwa watu wengine.
 • Osha mikono yako mara kwa mara.
 • Ikiwa unajisikia mgonjwa, kaa nyumbani. Usiende kazini.
 • Kohoa au kupiga chafya kwenye kitambaa au kiwiko.
 • Ikiwa una dalili zozote za virusi ya corona (COVID-19), lazima upimwe.
 • Kipimo cha virusi cha corona ni bure kwa kila mtu. Hii ni pamoja na watu wasio na kadi ya Medicare, kama vile wageni kutoka ng'ambo, wafanyakazi wahamiaji na wanaotafuta hifadhi.

Kwenye kurasa hii

Viwango vya sasa vya vizuizi katika Victoria

Mpango wa kupunguza vizuizi na hatua kwa Victoria kufika kwa hali ya kawaida ya COVID (COVID Normal) zimewekwa katika mpango wa kufungua tena wa Coronavirus (COVID-19) (Coronavirus (COVID-19) roadmap to re-opening).

Kuna mpango mmoja kwa mji mkuu wa Melbourne na mmoja kwa mikoa wa Victoria.

Afisa Mkuu wa Afya (Chief Health Oficer) anaweza kubadilisha vizuizi iwapo hali itabadilika.

Mji Mkuu wa Melbourne

Hatua ya Kwanza huanza saa 5 na dakika 59 usiku (11.59pm), 13 Septemba 2020 katika jiji kuu la Melbourne.

Kuna amri ya kutotoka nje wakati wa usiku kati ya saa 3 usiku (9pm) na saa 11 usiku (5am), na sababu nne tu za kuondoka nyumbani kwako:

 • Kununua chakula au vitu vingine muhimu
 • Zoezi (nje na kwa muda mdogo)
 • Kazi iliyoruhusiwa
 • Utunzaji, kwa sababu za huruma au kutafuta matibabu.

Kwa mazoezi na ununuzi wa vitu muhimu, lazima ukae ndani ya 5km ya nyumba yako.

Kuanzia wakati huu:

 • Amri ya kutotoka nje ni kuanzia saa 3 usiku hadi saa 11 asubuhi
 • Unaweza kutoka nyumbani kwako kufanya mazoezi kwa masaa mawili kwa siku.
 • Watu wawili wanaweza kukutana nje ya nyumba kwa muda usiozidi masaa mawili.
 • Ikiwa unaishi peke yako, au wewe ni mzazi pekee na watoto wote unaokaa nao wako chini ya umri wa miaka 18, unaweza kuchagua mtu mwingine ambaye anaweza kutembelea nyumba yako. Lazima awe mtu yule yule kila wakati. Unaweza pia kutembelea nyumba yake, ili mradi ni mtu mmoja mzima tu hapo kwenye nyumba wakati huo.
 • Viwanja vya michezo vinafunguliwa tena

Hatua ya pili: kutoka 28 Septemba 2020 - ikiwa kuna kesi mpya za coronavirus za kila siku 30-50 katika jiji kuu la Melbourne katika siku 14 hadi tarehe hii, na kutegemea ushauri wa wataalam wa afya.

Kuna sababu nne tu za kuondoka nyumbani kwako:

 • Kununua chakula au vitu vingine muhimu
 • Zoezi (nje kwa muda mdogo)
 • Kazi iliyoruhusiwa
 • Utunzaji, kwa sababu za huruma au kutafuta matibabu.

Kwa mazoezi na ununuzi wa vitu muhimu, lazima ukae ndani ya 5km ya nyumba yako.

Kuanzia wakati huu:

 • Hadi watu watano kutoka kaya mbili wanaweza kuonana nje.
 • Kutakuwa hatua za kurudi shuleni kwa wanafunzi wa Prep hadi Darasa la 2, VCE/VCAL na specialist schools katika Muhula wa 4.
 • Huduma ya watoto (childcare) inafunguliwa tena
 • Sehemu za kazi zaidi zinaweza kufungua.
 • Mabwawa ya nje hufunguliwa tena, mafunzo kwa mazoezi ya kibinafsi kwa hadi watu wawili kwa kila mkufunzi.
 • Mikutano ya kidini ya nje ya hadi watu watano na kiongozi mmoja wa imani inaruhusiwa.

Hatua ya Tatu: kutoka 26 Oktoba 2020 - ikiwa kuna wastani wa chini ya kesi mpya tano (kote jimboni) katika siku 14 zilizopita (kote jimboni), na ikiwa wataalam wa afya wanakubali.

Kuanzia wakati huu

 • Hakuna amri ya kutotoka nje na hakuna vizuizi vya kuondoka nyumbani au umbali unaoweza kusafiri.
 • Hadi watu 10 wanaweza kukusanyika nje
 • Unaweza kuwa na wageni watano nyumbani kwako kutoka kwa kaya nyingine. Lazima iwe nyumba sawa.
 • Wanafunzi wa Darasa la 3 hadi Darasa la 10 labda wanaweza kurudi shuleni ikiwa tuna idadi ndogo ya kesi na ikiwa wataalam wa afya wanakubali.
 • Maduka na watengeneza nywele hufunguliwa tena
 • Migahawa na mikahawa inaweza kufungua na huduma ya kuketi nje na kikomo cha kikundi cha watu 10.
 • Kurudishiwa hatua kwa hatua kwa michezo ya nje isiyo kwa kukumbana kwa watu wazima. Michezo ya nje itaanza tena kwa watu chini ya miaka 18 (kukumbana na kutokukumbana).

Hatua ya Mwisho: kutoka 23 Novemba 2020 - kutegemea ushauri kirasmi wa kiafya na ikiwa hakuna kesi mpya katika siku 14 zilizopita na wataalam wa afya wanakubali.

Kuanzia wakati huu:

 • Hadi watu 50 wanaweza kukusanyika nje.
 • Unaweza kuwa na hadi wageni 20 nyumbani kwako.
 • Maduka yote yako wazi.
 • Migahawa na mikahawa inaweza kufunguliwa na vikundi vya watu 20 tu kwa huduma ya kuketi ndani, na kikomo cha wateja 50 kwa jumla.
 • Michezo inaweza kuendelea, ikizingatia hatua za usalama. Michezo ya kukumbana itaanza kwa miaka yote.
 • Harusi na mazishi zinaweza kuwa na watu hadi 50 wanaohudhuria.
 • Ibada ya kidini ya umma inaanza tena, ikizingatia na sheria ya mita nne za mraba

COVID Kawaida (COVID Normal): ikiwa hakuna kesi mpya zinazotokea kwa siku 28, na hakuna kesi ambao ziko hai (kote jimboni), na hakuna kuzuka kwa kesi zinazoleta wasiwasi huko Australia, na wataalam wa afya wanakubali.

Kuanzia wakati huu:

 • Vizuizi hupunguzwa au kuinuliwa kuzingatia hali ya usalama.
 • Kuna hatua za kurudi kazini kwenye mahali pa kazi kwa watu ambao wamekuwa wakifanya kazi nyumbani.
 • Hakuna mipaka kwa ajili ya harusi au mazishi.
 • Hakuna mipaka juu ya mikusanyiko au wageni nyumbani.

Mikoa ya Victoria

Hatua ya Tatu: ikiwa idadi ya wagonjwa wapya iko chini ya watano (wastani katika nje ya miji) na hakuna mgonjwa mpya hata mmoja ambaye asili ya ugonjwa wake haijulikani (jumla katika nje ya miji) kwa muda wa siku 14 uliopita

Toka saa 5.59 usiku (11.59pm) tarehe 16 Septemba 2020 huko vijijini mwa Victoria:

 • Hakuna vizuizi vya kukuzuia usiondoke nyumbani au kwenda mbali nje ya miji katika Victoria.
 • Hadi watu 10 wanaweza kukusanyika nje.
 • Unaruhusiwa kuwa na wageni hadi watano nyumbani watakaokutembelea toka kwa kaya nyingine. Wageni wale watano lazima watoke kaya ile moja. Unaweza kuchagua kaya moja nyingine tu ambayo watu wake wanaweza kukutembelea. Huwezi kubadili kaya ile na kuchagua kaya nyingine. Watoto wachanga chini ya umri wa miezi 12 hawahesabiwi katika idadi ya kaya hizo.
 • Migahawa na mikahawa inaweza kufungua na huduma ya kuketi nje na kikomo cha kikundi cha watu 10.
 • Kuna kurudi kwa hatua kwa michezo ya nje isiyo ya kukumbatana kwa watu wazima. Michezo ya nje huanza tena kwa watu chini ya miaka 18 (kukumbatana na kutokubatana).

Hatua ya Mwisho: kutoka 23 Novemba 2020 - chini ya ushauri wa kirasmi wa kiafya na ikiwa hakuna kesi mpya (jimbo zima) katika siku 14 zilizopita na kutegemea ushauri wa wataalam wa afya.

Kuanzia wakati huu

 • Hadi watu 50 wanaweza kukusanyika nje.
 • Unaweza kuwa na hadi wageni 20 nyumbani kwako.
 • Maduka yote yanafungua.
 • Migahawa na mikahawa inaweza kufungua na huduma ya kuketi ndani kwa kikomo cha kikundi cha watu 20 na kikomo cha jumla ya kuketi cha watu 50.
 • Michezo inaweza kufungua, kutegemea na hatua za usalama. Michezo ya kukumbana inaanza kwa miaka yote.
 • Harusi na mazishi zinaweza kuwa na watu hadi 50 wanaohudhuria
 • Ibada ya kidini ya umma inaanza tena, ikizingatiwa na sheria ya mita nne za mraba

COVID Kawaida (COVID NORMAL): ikiwa hakuna kesi mpya zinazotokea kwa siku 28, na hakuna kesi ambao ziko hai (kote jimboni), na hakuna kuzuka kesi zinazoleta wasiwasi huko Australia.

Kuanzia wakati huu

 • Vizuizi hupunguzwa au kuinuliwa, kutegemea hali ya usalama
 • Kuna hatua za kurudi kazini kwenye mahali pa kazi kwa watu ambao wamekuwa wakifanya kazi nyumbani,
 • Hakuna mipaka kwa ajili ya harusi au mazishi
 • Hakuna mipaka juu ya mikusanyiko au wageni nyumbani

Jinsi ya kukaa salama na wenye afya

Coronavirus (COVID-19) bado iko nasi na inaweza kuenea haraka. Ili kusaidia kuweka familia zetu na jamii salama, sote lazima tufanye sehemu yetu.

Hapa kuna mambo rahisi unayoweza kufanya ili uwe salama:

 • Osha mikono yako na sabuni na maji kwa angalau sekunde 20.
 • Kohoa na kupiga chafya kwenye tishu au kiwiko.
 • Jiweke umbali wa usalama wa angalau mita 1.5 kutoka kwa watu wengine.
 • Vaa kifuniko cha uso juu ya pua na mdomo ikiwa itakubidi utoke nyumbani.
 • Nenda kwenye uchunguzi wako wa kimatibabu.
 • Ikiwa unajisikia mgonjwa, kaa nyumbani. Usitembelee familia au uende kazini.
 • Pimwa ikiwa una dalili zozote kisha nenda moja kwa moja nyumbani.

Msaada unapatikana

Ikiwa una wasiwasi juu ya kupoteza mapato wakati unasubiri matokeo yako ya vipimo, unaweza kustahiki $450 coronavirus (COVID-19) Malipo ya Kutengwa.

Ikiwa unapimwa na unayo coronavirus au uliwasiliana karibu na kesi iliyothibitishwa, unaweza kustahiki malipo ya $1,500. Kwa habari zaidi piga simu kwa Coronavirus Hotline kwa 1800 675 398. Ikiwa unahitaji mkalimani, bonyeza sifuri (0).

Ikiwa wewe au mtu unayemjua ana wasiwasi au ana maswali, unaweza kupiga Lifeline kwa 13 11 14 au Beyond Blue kwenye 1800 512 348. Ikiwa unahitaji mkalimani, kwanza piga simu 131 450.

Ikiwa unahisi kutengwa, unaweza kupiga simu ya coronavirus (COVID-19) kwa simu ya 1800 675 398 na ubonyeze tatu (3). Utaunganishwa na mtu wa kujitolea kutoka Msalaba Mwekundu wa Australia ambaye anaweza kukuunganisha na huduma za misaada wa karibu.

Vifuniko vya uso

Kila mkaaji wa Victoria wa miaka 12 na zaidi lazima avae kifuniko cha uso wakati wa kuondoka nyumbani, isipokuwa akiwa na sababu ya kisheria ya kutofanya hivyo. Kwa mfano:

 • ikiwa una ugonjwa fulani kama hali mbaya ya ngozi kwenye uso wako, au shida ya kupumua
 • ikiwa uko kwenye gari, peke yako au na mtu kutoka kwa kaya yako
 • ikiwa unafanya mazoezi mazito, lakini ni lazima ubebe kifuniko cha uso.

 

Upimaji na kutengwa

Ikiwa una dalili zozote za coronavirus (COVID-19), lazima upimwe na ukae nyumbani hadi upate matokeo yako. Usiende kazini au madukani.

Dalili za coronavirus ni pamoja na:

 • Homa, baridi au jasho
 • Kikohozi au maumivu koo
 • Upungufu wa kupumua
 • Pua lenye makamasi
 • Kupoteza hisia ya harufu au ladha

Kipimo cha coronavirus (COVID-19) ni bure kwa kila mtu. Hii ni pamoja na watu wasio na kadi ya Medicare, kama wageni kutoka ng'ambo, wafanyakazi wahamiaji na wanaotafuta hifadhi.

Ikiwa utapimwa na una coronavirus (COVID-19), lazima ujitenge nyumbani kwako. Kwa habari zaidi angalia Nini cha kufanya ikiwa umepimwa una coronavirus (COVID-19) (Word).

Ikiwa wewe ni mtu wa mawasiliano ya karibu ya mtu aliye na coronavirus (COVID-19) lazima ujitenge kwa siku 14. Kwa habari zaidi angalia Nini cha kufanya ikiwa umekuwa ukiwasiliana kwa karibu na mtu aliye na coronavirus (COVID-19) (Word).

Rasilimali

Tafadhali tumia maelezo hapa chini na uyashirikishe na jamii yako kwa barua pepe, mtandao wa kijamii au njia zingine za kuw.

Kupimwa na kujitenga

Kukaa salama

Kupata msaada

Vifuniko vya uso